Darasa ni la Digital
Electronics na sielewi analolifunza mwalimu.Usitake* jua wivu ninao kwa
wanagenzi wenzangu wanaolielewa somo hili ninavyoelewa kula. Sijui kama ni kwa
sababu sina raha na cheti ninachokitafuta hapa, kawaida yangu ama ni siku tu
isiyo njema kwangu. Hilo halihusishi sana. Nilipokuwa nimezubaa wazo likanijia
la kuandika nukuu hii kwa Kiswahili. Sio kawaida, hata ninavyohisi ni kama
wazimu wa aina fulani. Nilitumia Kiswahili andishi miaka kama saba hivi
iliyopita. Mimi ni mojawapo ya wale ambao Kiswahili hutatiza wakati ufikapo wa
kukiandika na kujieleza. Matumizi ya lugha pia nashuku nimekiuka sheria kadha nabado
nitaendelea kizikiuka niendeleapo na makala haya. Siwezi andika ng’ano ya maana
sana vile nikitumia hii lugha kwa sababu, wengi hawataelewa, lakini kwa sababu
fikra hiyo imenipata, lazima ningejipa motisha na niandike kwa lugha ya Kiswahili.
Pale mwanzo sijui nilitoa wapi hilo wazo la
kutumia lugha hii,lakini nimekumbuka sasa…. Leo nimekuwa tu nimejipoteza kwa
mawazo, na nikafikiri kunukuu mawazo hayo kwa mtandao nikipitia Facebook na
Twitter. “Huu ndio mwezi ulioanza kama
nimeinua mkono na kulingana na maono, utaisha nikiwa hivo hivo – Julai”. Wazo
lingine likafuata kuwa,watakaosoma watabaki wameshangazwa na tamko hilo
(Kawaida yao) Nilitupilia wazo hilo mbali na mahali lilipoanguka, wazo la
kuandika nukuu kwa lugha ya Kiswahili likanipata. (Samahani lakini, kila wakati
najipata nimeandika ‘Kishwahili’)
Ukiwa makini utapata sina la maana vile la
kueleza, katika aya ya kwanza. Usiwe na wasi wasi. Uzuri wa kuwa mwandishi ni
kuwa, unaposhika kalamu na karatasi, mawazo huanza kutiririka. Kwa wanaoshangazwa
na wazo la leo ambalo sikulituma kwa Facebook na Twitter, nilimaanisha kuwa
mwezi huu, ulianza ukiwa na changamoto tele. Sio kipesa ya matumizi, sio kikazi,
sio kibiashara, sio kimapenzi, sio kwa marafiki… nabado zaendelea kuongezeka.
Shida ni mingi kiwango ambacho hata baridi ya Julai siwezi ihisi kwani nimekuwa
kiguu na njia jasho likinitiririka kote kote nikijaribu kukaza mambo yaniendee
vyema. Usitie shaka, hiki sio kilio. Sitaki kutumia jina shida,kwani shida ni
kujaza akili na fikra mbaya ambazo napenda kuepuka. Yaani mtazamo hasi wa akili.
(Negative Mental Attitude)
Hapo awali nilijaribu kueleza ugumu wa kujieleza
kwa Kiswahili. Wengi huwa hawapendi kuisoma lugha hii na ndio kwa sababu
nitakoma kuandika makala haya hivi karibuni. Lakini wasomaji wakipenda
nitaendelea tu. Hakuna namna (‘Kijeshi’)
Nikimalizia, nimeamua kujipa motisha wa kuandika
ili niwe na nidhamu ya kumaliza ninayoyaanza. Hii ni mojawapo ya malengo ambayo
nimeyanukuu kutekeleza mwaka huu. Kwenye orodha ya makala yanayongoja
kuendelezwa ni Visa vya Liam, How I Joined The Military, na Career Path.
Endelea kuburudika Msomaji mpendwa.
Endelea kuburudika Msomaji mpendwa.
Cool!
ReplyDelete